GUARDIOLA, MOURINHO UPINZANI KAMA SPAIN
KOCHA ATETEA KIDOLE CHA DELE ALLI
Kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino amesema mchekeshaji, Mr. Bean atapaswa afungiwe asionekane kwenye televisheni kama staa wake Dele Alli ataadhibiwa kutokana na kitendo chake cha kuonyesha kidole cha kati. Dele alifanya tukio hilo katika mechi ya kimataifa kati ya England na Slovakia iliyofanyika Jumatatu iliyopita.
Pochettino amemtetea kiungo wake na kusema huo ni utani aliokuwa akiuelekeza kwa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Kyle Walker, ambaye walikuwa pamoja Spurs kabla ya beki huyo wa pembeni kuhamia Manchester City kwenye dirisha lililopita. Lakini, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) linadai kwamba Dele alifanya hivyo kumlenga mwamuzi, Mfaransa Clement Turpin na uchunguzi zaidi umeanza kufanyika.
MASHABIKI MAN UNITED WAMUOMBA POGBA AMSHAWISHI THOMAS LEMAR
Mashabiki wa Manchester United, wamemuomba mshambuliaji wao Paul Pogba kumshawishi Mfaransa mwenzake, Thomas Lemar kuhamia klabuni hapo dirisha la usajili msimu wa Januari.
Mashabiki hao walisema licha ya dirisha la usajili kufungwa lakini Pogba anaweza kuendelea kumshawishi Lemar kuweka akilini kuhusu Manchester United.
Lemar ameacha kilio Arsenal baada ya kuwakatalia kujiunga nao kwenye usajili wa kiangazi uliofungwa Agosti 31 saa 6:00 usiku.
Arsenal walikuwa tayari kulipa Pauni 92 milioni kumpata mshambuliaji huyo wa Monaco, hata hivyo mpango huo ulikwama dakika za mwisho za usajili.
Lemar mwenye miaka 21 aliweka bayana kwamba hataki kuichezea klabu ambayo inashiriki Ligi ya Europa, ambapo Arsenal ndiyo itashiriki mashindano hayo.
Pogba walikutana na Lemar kwenye timu yao ya Taifa ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Uholanzi mechi ya kufuzu Kombe la Dunia.
Baada ya ushindi huo wa juzi, Pogba alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Istagram pamoja na picha akiwa na Lemar akisema kuwa atamshawishi kujiunga na klabu hiyo msimu ujao huku mashabiki wakimuomba kufanya hivyo.
LACAZETTE ATUA RASMI ARSENAL
Hatimaye Alexandre Lacazette ametua Arsenal baada ya kukamilisha mipango ya uhamisho wake wenye thamani ya Pauni 52 milioni kutoka Lyon.
Lacazette, 26 aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal jana mchana tayari kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Nyota huyo aliyeifungia klabu yake, Lyon mabao 37 msimu uliopita atalipwa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Huo, utakuwa usajili kwa kwanza mkubwa wa kocha Arsene Wenger ambaye ana kibarua cha kuwabakisha kundini waasi Hector Bellerin na Alexis Sanchez wanaotaka kuondoka.
Mshambuliaji huyo Mfaransa anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Arsenal na pengine atamwondoa Olivier Giroud anayetakiwa na klabu kadhaa za England, West Ham na Everton.
Rais wa Lyon, Jean- Michel Aulas alisema juzi kuwa uhamisho wa Lacazette ambaye alitambulishwa kwa wenzake waliowasili kuanza maandalizi ya msimu mpya, utakamilika ndani ya saa 48.
Aulas alitamba kuwa ni faraja kuona mchezaji wao amenunuliwa kwa zaidi ya Euro 45 milioni.
PEPE ATUA RASKI BESIKTAS YA UTURUKI
Mchezaji wa Real Madrid, Pepe amekamilisha mipango yake ya kuhamia Uturuki baada kusajiliwa na klabu ya Besiktas.
Mreno huyo mwenye miaka 34 awali alikuwa akihusishwa kujiunga na PSG kabla ya kubadili mawazo ya kwenda Besiktas.
Tangu ajiunge na FC Porto mwaka 2007 kwa dau la Pauni 26 milioni, raia huyo wa Brazil amecheza michezo 334 huku akifunga mabao ya aina yake 15 na ametoa pasi 19 za mabao.
REAL YAWEKA DAU LA REKODI KWA HAZARD
Real Madrid ipo tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa kutoa pauni 100milioni ili kumchukua Eden Hazard.
Mabingwa hao wa Hispania wanalengo la kuimarisha kikosi Zinedine Zidane bila ya kujari nini kitakachotokea katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumamosi dhidi ya Juventus.
Pia, wanampango wa kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea, lakini lengo lao kubwa ni kumnasa winga wa Chelsea, Hazard.
Real kwa muda mrefu wamekuwa akimfuatilia Mbelgiji huyo kwa lengo la kumuondoa Stamford Bridge.
Real imeweka wazi kuwa inataka kutumia dau nono kumsajili Hazard kwa kuvunja rekodi ya uhamisho wa 100milioni ili kumuondoa Stamford Bridge.
Hazard amehakikisha kupewa nafasi ya kucheza kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Real, akicheza kati ya washambuliaji watatu Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale.
Hata hivyo, Hazard amesisitiza kuwa bado anafuraha kuwa London, lakini Real inaamini wataweza kumsajili kutokana na heshima ya nyota huyo kwa Zidane, ambaye amekuwa akimwangalia na kutamani kuwa kama yeye.
✩✩✩✩✩ CHELSEA MABINGWA EPL 2016/2017 ✩✩✩✩✩
CONTE ACHAGULIWA KUWA KOCHA BORA WA MWAKA EPL
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ametunukiwa tuzo ya kocha bora Bodi ya Ligi Kuu England.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa Italia na Juventus, amepata tuzo hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa baada ya kukiongoza kikosi cha Chelsea kutwaa ubingwa msimu wa 2016/17.
Ubingwa wa Chelsea ulianza kunukia tangu Machi baada ya kuanza kuchanja mbuga, huku wakiziacha timu zilizokuwa zinaifuatia kwa pointi nyingi.
Chelsea imemaliza mashindano hayo ikiwa imekusanya pointi 93 na kushinda michezo 30 kati ya 38 ilyocheza msimu huu.
Hata hivyo, Conte ana nafasi ya kutwaa taji jingine la ndani kutokana na kuwa na mechi ya fainali ya Kombe la FA Jumapili wiki hii.
Chelsea watakuna na Arsenal kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali kwenye dimba la Wembley.
TERRY AONDOKA CHELSEA KWA KUMWAGA CHOZI BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA
5-1 ni matokeo aliyoyapata Chelsea katika mechi yake ya mwisho ya msimu wa 2016/2017 dhidi ya Sunderland katika uwanja wao wa Stamford Bridge.
Magoli hayo yalifungwa na Willian dakika ya 8, E. Hazard dakika ya 61, Pedro dakika ya 77 na Batshuayi dakika ya 90 na 92.
Terry na Diego Costa walitumia nafasi hiyo kuwaaga mashabiki wa Chelsea.
Harry Kane ameibuka mfungaji bora na Delle Ali mchezaji bora chipukizi huku tuzo zingine zikichukuliwa na Chelsea kupitia kwa; Hazard mchezaji bora, Thibaut golikipa bora, na Kante akijipatia tuzo 2 binafsi za uchezaji bora kwa makocha na waandishi wa habari.
Hadi sasa timu zilizopo 4 bora ni Chelsea, Tottenham, Manchester City na Liverpool iliyopokonywa nafasi yake na Man United baada ya kuifunga Ajax na kufuzu UEFA..
Matokeo ya Mzunguko wa Mwisho Kiujumla:
MAN UNITED:
Kusajili wanne tu.
Klabu ya Manchester United imedokeza usajili wake utahusisha wachezaji watatu au wanne tu ambao ni maalumu kwenye nafasi ya mshambuliaji, mabeki wa kati na viungo.Uongozi wa klabu hiyo ulitoa taarifa kwamba watafanya kama walivyofanya miezi michache iliyopita kwa Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba.
Kocha Jose Mourinho alisema suala la usajili klabuni hapo linapaswa kufanyika kwa mkakati maalumu kulingana na mahitaji halisi.
Hata hivyo BBC Sport lilieleza kwamba mipango ya Mourinho huenda imelenga zaidi kupata saini ya wachezaji kama Griezmann, Andrea Belotti, Michael Keane na Victor Lindelof.
United imeachia jezi mpya watakayoitumia ugenini msimu ujao 2017/2018.
TOTTI ASTAAFU AKIUPENDA MPIRA
Kiungo Francesco Totti amesema "mapenzi yake kwa soka hayana mwisho" wakati akijindaa kwa mara ya mwisho kuvaa jezi ya Roma Jumapili ijayo dhidi ya Genoa.Totti mwenye miaka 40, ameamua kustaafu baada ya kucheza soka kwa miaka 24 na kuwa mkurungezi katika klabu yake hiyo.
Katika maisha yake ya soka amefunga mabao 307, katika mechi 783 alizocheza yangu alipoanza kuichezea Roma mwezi Machi1993 akiwa na miaka 16.
"Siwezi kusema kwa kifupi hii rangi inamaana gani kwangu, inachomanisha siku zote kitamaanisha," aliandika katika tweeted.
"Ninachohisi ni mapenzi yangu katika soka hayatakwisha. Siwezi amini kwamba sitaweza tena kucheza.
"Kuanzia Jumatatu nipo tayari kuondoka. Nipo tayari kwa changamoto mpya. Roma dhidi ya Genoa, Jumapili, 28 Mei 2017, itakuwa mechi yangu ya mwisho kuvaa jezi ya Roma."
Totti, ametwaa Kombe la Dunia akiwa na Italia 2006, ameshinda taji moja la Serie A na makombe mawili ya Coppa Italias akiwa na Roma.
N'GOLO KANTE na tuzo zake mbili !
Mchezaji wa Chelsea, N'golo Kante alishinda tuzo binafsi ya mchezaji bora wa mwaka wa waandishi wa habari kwa msimu wa 2017-2018 kwa kura za waandishi wa habari.
Kama ilivyokua kwa ile ya mwezi uliopita, kura zake zilifuatiwa kwa karibu na Eden Hazard huku Delle Alli akishika nafasi ya tatu na wengine waliokuwepo ni Zlatan Ibrahimovic, Romelu Lukaku, Alexis Sanchez na Hary Kane.
Miezi kadhaa iliyopita;
Frank Lampard alisema, "Kiungo bora duniani." na Alan Shearer alisema yakuwa, "Nadhani mtakua mnamtazama mchezaji bora wa msimu wa waandishi wa habari na mchezaji bora wa msimu wa wachezaji." magwiji hao wa soka walikua wakimzungumzia Ng'olo Kante.
Delle Ally aliibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora kijana wa msimu ni nafasi ya pekee ambayo kwa umri wake na uwezo wake amestahili. Aliwashinda Lukaku, Hary Kane, Leroy Sane wa Machester City, mlinzi wa kati wa Burnley, Michael Keane na golikipa wa Sunderland, Jordan Pickford.
1) Kufunga magoli mengi zaidi.
2) Kuruhusu magoli machache zaidi.
3) Kuwa na mchezaji mwenye uwezo wa kufunga zaidi ya magoli 20.
4) Kuzishinda timu unazokumbananazo ikiwa ni kubwa au ndogo.
5) Kuwa na makocha waliopata mafanikio kipindi cha uchezaji wao.
6) Kuwa na kikosi chenye wachezaji wazoefu na vijana.
7) Kugharamika katika kusajili.
8) Kupiga mashuti mengi golini.
9) Kuwa na nidhamu nzuri.
10) Kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa.
11) Kushinda penati nyingi.
LA LIGA
Real Madrid inayoongoza kwa alama 3 ina nafasi nzuri ya kubeba ubingwa ingawa ina mchezo mgumu dhidi ya Malaga. Huku Barcelona ikiwa na mchezo mwepesi dhidi ya Eibar.
Barcelona inategemea miujiza ya kulingana pointi na kunyakua ubingwa kwa kigezo cha kuifunga magoli mengi Real Madrid ilipokutana nayo.
UEFA
FAINALI JUNI 3, 2017
Juventus na Real Madrid zitakutana katika fainali baada ya timu zote kuvuka katika nusu fainali.
Fainali itafanyika Wales katika uwanja wa taifa wa Cardiff Juni 3 (tarehe 3 ya mwezi wa 6) 2017.
Endapo Real Madrid ikishinda itakua timu ya kwanza kutetea taji la UEFA baada ya miaka 27.
FIFA
FIFA YACHUNGUZA UHAMISHO WA POGBA
Nyon, Uswisi. Uhamisho ghari wa kiungo, Paul Pogba umezua jambo baada ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuamua kufanya uchunguzi.
Fifa inataka kujua kuhusu malipo anayotakiwa kupewa wakala wa Mfaransa huyo Mino Raiola inayodaiwa kupokea kamisheni ya pauni 41.39 milioni.
Pogba alinunuliwa kwa pauni 89 milioni kilicholipwa na Manchester United kumtoa Juventus kilizua mjadala mwishoni mwa wiki hii.
Msemaji wa Fifa, alisema kwamba, "Tunathibitisha kwamba ni kweli tumeomba taarifa za uhamisho wa mchezaji huyo ili kuweza kufuatilia suala hilo."
Uhamisho wa mchezaji huyo ndiyo ghari kufanyika duniani ambapo alivunja rekodi ya uhamisho wa Gareth Bale kutoka Tottenham aliochukuliwa na Real Madrid kwa dau la pauni 86 milioni.
Fifa imekuwa ikiomba taarifa zaidi juu ya uhamisho huo.
Msemaji wa Man United amethibisha kwamba Fifa walipewa taarifa zote wakati Pogba akihamia England.
Alisema: "Sitaweza kuzungumzia kuhusu mkataba wake, Fifa inataarifa zote tangu ulipofanywa uhamisho wake Agosti."
Taarifa kutoka Ufaransa zinadai kuwa Fifa imekuwa ikichunguza uhamisho huo Pogba tangu Septemba 16.
Inaaminika kwamba wanaangalia suala la ummiliki wa tatu jambo ambalo limepigwa marufuku England.
Raiola alikataa kuzungumzia suala hili, lakini awali alikata madai ya Pogba kumilikiwa na watu watatu, japokuwa alidai Juventus siyo wamiliki wa haki za matangazo ya mchezaji huyo.
















Duh mungu azilaze Roho za marehemu maala pema peponi.
ReplyDelete