Tuliweza kukutana na
kuwa na lengo moja, la kufanyia kazi ndoto zetu nzuri kwa kujitoa kikamilifu
kwa hali na mali. Haikuwa kazi rahisi hata kidogo kuhakikisha tunakua pamoja.
Mnamo tarehe 1 mwezi wa
6 mwaka 2016 kikundi kilianza rasmi kikiwa na watu 8 kwa jina la Youth
Unlimited Dream Exploration Group (YUDE).
Kikundi hiki
kinashughulika na ndoto za vijana zinazolenga kuleta maendeleo katika jamii.
Hivyo kwa pamoja YUDE ni kikundi cha vijana wanaothubutu kujishughulisha ama kutumia
fursa zilizopo na kutengeneza nyingine kuleta maendeleo katika jamii kwa
kutumia taaluma zao na vipawa vyao mbalimbali katika nyanja zote.
Malengo:
- · Kuamsha vijana kutimiza ndoto zao kwa kujitoa kikamilifu.
- · Kufanya miradi mbalimbali zaidi kwa kuhusisha teknolojia.
- · Kuwa na mfumo mzuri wa taarifa kwa jamii.
- · Kuleta mahusiano mazuri kati ya vijana na jamii.
- · Kutumia fursa zilizopo katika jamii kuleta maendeleo.
Shughuli
zetu:
- · Kikundi.
Ø Kutumia
fursa za IT kama vile kutengeneza na kuiendesha mifumo mbalimbali (blog/
website, IT Systems), kufundisha na kushauri.
Ø Kutumia
fursa za ujasiliamali kufanya miradi mbalimbali na kuisadia jamii kupata elimu
ya ujasiliamali.
- · Kijamii.
Tunajitoa
kikamilifu kuisaidia jamii katika shughuli mbalimbali kama vile elimu, usafi na
kutembelea wagonjwa ama wenye shida mbalimbali. Pia kutoa habari za matukio mbalimbali
za ndani na nje ya jamii.
Miradi:
Ipo miradi ambayo
inahitaji msaada wa hali na mali (Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi).
Changamoto:
- · Kutokua na mtaji wa kutosha.
Sehemu
kubwa ya vijana hawana ajira, hivyo ni vigumu kutegemea kipato cha ndani pekee
kutimiza malengo.
- · Ugumu wa kuwapata vijana wote kwa wakati mmoja, kutokana na kazi zetu nyingi kuwa ni za kujitolea na zisizo na kipato cha kutosha.
- · Mtazamo hasi wa wanajamii walio wengi juu ya vijana.
- · Upungufu wa vitendea kazi hususani katika maswala ya Teknolojia (Kompyuta, kamera n.k)
- · Ukosefu wa udhamini.
Maombi:
- · Tunaomba misaada ya hali na mali katika fursa tunazozichukua.
- · Tunapokea kazi za kibiashara kama vile ajira, fursa ya kuweka matangazo katika mitandao yetu n.k
- · Tunakaribisha mawazo ama michango mbalimbali kutoka katika jamii.
Hitimisho:
Tunaomba ushirikiano
zaidi kutoka kwa serikali, watu binafsi ama mtu yeyote mwenye mapenzi mema
kiujumla.



0 comments:
Post a Comment