KITAIFA: Brazil yaisamehe Tanzania mabilioni ya fedha ya mwaka 1979. Kamanda Mambosasa amtaka polisi anayejiita Faru john. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa akamatwa na polisi baada ya kumkaribisha mkuu wa mkoa kwenye kikao cha kijiji akiwa amelewa. Bunge lahitimishwa watanzania wakishuhudia kheri na vitimbwi. Kina Manji wasomewa mashtaka saba wakiwa muhimbili. Sakata la mimba shuleni latua kwa ma-DC. Majaliwa: Marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi. Bakwata yalaani mauaji Kibiti. JPM kuzindua viwanda Pwani leo katika ziara ya siku 3 inayoanza mkoani humo. Kamusi Kuu ya kiswahili yapitishwa Bungeni. ********** KIGAMBONI: Hali ya hewa ni ya baridi kiasi na upepo, wananchi washauriwa kuwa makini na upepo, vumbi wakati wa mchana na baridi wakati wa usiku. **********KIMATAIFA: Boti yazama, 6 wafa, 20 wakimbizwa hospitali Colombia. **********BIASHARA: Sekta ya Benki yaanza kuona nuru mpya. Rangi itakuongezea au kukupunguzia wateja katika biashara yako. Mazingira ya biashara yaboreshwe kukuza uchumi, kuondoa umasikini. Shilingi 50 yaanza kupoteza bidhaa za kuendananazo baada ya wafanyabiashara wengi kutengeneza zaidi vitu vya shilingi 100. *********MICHEZO: *** UEFA: Timu za EPL zaanza vyema mzunguko wa kwanza. Diego Costa aachwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa chelsea watakaoshiriki UEFA hatua ya makundi. Zlatan Ibrahimovic ajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa Man United watakaoshiriki UEFA hatua ya makundi. Real Madrid bingwa. ENGLAND: Chelsea bingwa EPL, Conte achaguliwa kocha bora wa msimu. . ******** LA LIGA: Real Madrid bingwa la liga. ******* USAJILI: Lacazette kumfikirisha upya Sanchez juu ya kuihama Arsenal. Atletico yamtaka Diego Costa kutulia Chelsea hadi Januari.*********** AFRIKA: Ligi ya vilabu bingwa Afrika iko katika hatua ya makundi. AFCON 2017; Cameroon alitawazwa kuwa Bingwa baada ya kuifunga Misri goli 2-1 katika fainali na sasa inacheza kombe la mabara. ******** Pata habari hizi na nyinginezo nyingi kupitia habari zetu za michezo za kimataifa. ********. TANZANIA: *** Simba yazidi kufanya kweli. Msuva aipaisha TZ. TRA: Klabu za soka zilipe kodi. *** KIGAMBONI: Uhaba wa ligi ndani ya Wilaya ya Kigamboni umezorotesha uibuaji wa vipaji na kudumaza viwango vya wachezaji waliopo. Wadhamini waombwa kujitokeza kuanzisha ligi mbalimbali wilayani humo ili kuwaokoa vijana wengi na mambo mabaya. Katika uwanja wa Mnadani karibu na maeneo ya Tungi kwa kasilati ligi ambayo inakusanya wachezaji wengi kwa sasa imeisha kwa Mkunazini kuibuka bingwa katika fainali baada ya miaka mingi kupita. Ligi ya Eid El Fitr yaendelea katika hatua ya robo fainali leo 20/6/2017, katika uwanja wa machava.

DONDOO ZA USAJILI BARANI ULAYA

ANTONIO RUDIGER
Chelsea imefikia makubaliano na Roma juu ya beki wa kati Antonio Rudiger kujiunga na Chelsea msimu ujao.
Ikumbukwe beki huyo mwenye miaka 24 aliisaidia Ujerumani kubeba ubingwa wa kombe la dunia la mabara huko Urusi wiki iliyopita baada ya kuifunga Chile kwa goli 1-0.
Mchezaji huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii nchini marekani, na ada ya usajili inakadiriwa kuwa ni paundi 34.


RAMY BENSEBAINI
Klabu ya AC Milan imetangaza nia ya kumsajili Mualgeria Ramy Bensebaini kwenye kikosi chao msimu wa 2017/18.
Gazeti la Dello Sport liliripoti kwamba mchezaji huyo wa Stade Rennais  ni miongoni mwa wachezaji watano wa Ligue 1 wanaohitajika kusajiliwa AC Milan.
Wachezaji wengine wanaohitajika ni Presnel Kimpembe kutoka PSG ambaye ni Mfaransa mzaliwa wa DRC, Toulouse Issa raia wa Ufaransa mzaliwa wa Senegal na Emmanuel Mammana  kutoka  Olympique Lyon pamoja na Mouctar Diakhaby ambaye ni Mfaransa mzaliwa wa Guinea.


DANI CEBALLOS
Makamu wa Rais wa klabu ya Real Betis, Lorenzo Serra amethibitisha vita iliyoibuka baina ya klabu vigogo za Hispania katika mbio za kuwania saini ya mchezaji wake, Dani Ceballos (21).
Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kuondoka kikosini Real Betis msimu huu wa kiangazi.
Mtandao wa Goal ulieleza kuwa, licha ya majadiliano yanayoendelea,  nafasi kubwa kwa mchezaji huyo ni kubaki Real Betis.
Hata hivyo, vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kuwa Ceballos aliwaeleza ndugu zake wa karibu kuwa anapenda zaidi kujiunga na Barcelona kuliko Real Madrid.


ALEX SANDRO
Beki wa Juventus, Alex Sandro amefikia makubaliano binafsi na Chelsea na sasa wakati wowote atajiunga  Stamford Bridge.
Beki huyo wa Juventus atajiunga na Stamford Bridge kwa gharama ya pauni 60 milioni baada ya Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka.
Baada ya ofa ya pauni 45 milioni iliyokataliwa na  Juve 'Old Lady', sasa kocha Antonio Conte yuko tayari kuja na dau jipya.
Kwa mujibu wa gazeti la Italia, Corriere delle Sera, Mbrazili huyo mwenye miaka 26, anahamu kubwa ya kuhamia London, lakini kama mabingwa hao wa Serie A watakuwa tayari kupokea pauni 60 milioni.
Calcio Mercato awamedai kuwa Sandro amehaidiwa mshahara wa pauni 6 milioni kwa mwaka endapo atasaini Chelsea, hasa baada ya kukataa kusaini mkataba mpya Juventus.
Taarifa zinadai miamba hiyo ya Italia tayari imeshaanza kuangalia wachezaji wa kuziba pengo lake ambao ni Benjamin Mendy wa Monaco, pamoja na Matteo Darmian wa Manchester United.


CONTE
Kocha mkuu wa Chelsea anakaribia kuongeza mkataba utakaomfanya kuwa kocha anayelipwa zaidi ya makocha wengine katika historia ya waliowahi kupita klabuni hapo kwa kuifundisha timu hiyo baada ya mazungumzo na uongozi kufikia pazuri.
Conte ni kocha makini zaidi kwenye usajili.
Romelu Lukaku, Timoue Bakayoko, Marco Verati na Daniel Alves ni kati ya majina yaliyoibuka hivi karibuni wakihusishwa na Chelsea.


EDERSON
Ederson amekuwa kipa ghali zaidi baada ya kusajili na Manchester City akitokea Benfica kwa gharama ya pauni 34.9 milioni.
Uhamisho wa Ederson unavunja rekodi ya uhamosho wa kipa Gianluigi Buffon aliyesajili kwa pauni 33 milioni wakati akitoka Parma kwenda Juventus mwaka 2001.
Taarifa ya Benfica ilithibisha kuwa Ederson anajiunga na Manchester City kwa uhamisho ilivyovunja rekodi ya dunia ya pauni 34.9 milioni.
Kipa huyo mwenye miaka 23, anakuwa mchezaji wa pili kusajili wa Pep Guardiola msimu huu baada ya kumnasa kiungo wa Monaco, Bernardo Silva wiki iliyopita.
Mbrazil huyo bado hajaichezea timu yake ya taifa, lakini ameitwaa katika kikosi kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi Argentina na Australia.


ATLETICO MADRID
Klabu ya Atletico Madrid imeangukia pua kutokana na rufaa yake kukataliwa na mahakama inayoshughulikia masuala ya michezo.
Timu hiyo ilikata rufaa yake kupinga kufungiwa kufanya uhamisho na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) hadi mwakani.
Kocha wa Atletico Madrid,  Diego Simione na wenzao Real Madrid walifungiwa kufanya usajili kwenye madirisha mawili ya usajili kutokana na kwenda kinyume na kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni chini ya miaka 18.
Baada ya kushindwa rufaa hiyo Fifa, Atletico waliukosa usajili wa Januari mwaka huu kutokana na kutumikia adhabu hiyo.
Hata hivyo, Atletico hawakukata tamaa na kuamua kukata rufaa ambayo imetupiliwa mbali huku wakitakiwa kuendelea kutumikia adhabu hiyo hadi msimu wa mwaka 2017-18 ili kukamilisha na dirisha la pili la usajili.
Kwa uamuzi huo, utamwathiri mchezaji wake Antonio Griezmann aliyekuwa akitakiwa na Manchester United. Pia upande wao Atletico wamezika ndoto ya kuwasajili Alexandre Lacazette kutoka Lyon, Diego Costa kutoka Chelsea.
Hivi karibuni Griezmann amekuwa kwenye joto la usajili baada ya Manchester United kupanda dali la Pauni 70 milioni, huku timu yake ikionyesha kutaka dau la Pauni 100 milioni.


BERNARDO SILVA
Manchester City imefanya usajili wake wa kwanza kwa kumsajili kiungo wa Monaco, Bernardo Silva mwenye miaka 22. City ilipata nafasi nzuri ya kuridhishwa na uwezo wake katika mechi ya klabu bingwa dhidi ya Monaco ambayo iliibuka na ushindi wa 3-1 na kufanikiwa kusonga mbele. Mchezaji huyo ambaye ameifungia Monaco magoli 8 msimu wa 2016/2017 katika michezo 36 anatarajiwa kutua kikosini tarehe 1/6/2017 na atavaa jezi namba 20.
Pia City inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji Aubameyang wa Dortmund.


MOHAMED SALAH
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha nia ya kuihitaji huduma ya mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye anaichezea timu ya Roma, Mohamed Salah mwenye miaka 24 kutoka Misri. Ikumbukwe Liverpool walitaka kumsajili kipindi cha nyuma kabla ya Chelsea kuingilia katikati na kuwazidi maarifa ya usajili Liverpool.
Pia Liverpool inamfuatilia kwa karibu kiungo wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain, huku uongozi ukiwa umempatia Klopp rungu la kumfuatilia Aubameyang.


SANCHEZ
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Franck Ribery huenda akatimka klabuni hapo baada ya kucheza kwa miaka 10 ikiwa Alexis Sanches atasajiliwa msimu huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Le10Sport,  Kiungo huyo mkongwe wa Ufaransa  ataachiwa na klabu yake na anatarajiwa kutua kwenye ligi ya Ufaransa mambo yakimuendea vyema.
Hata hivyo, uhamisho huo umekuwa na pande mbili zinazotegemeana kwani mchezaji huyo ataondoka iwapo dili la kumsajili Sanchez litakamilika.
Licha ya kupata majeraha, lakini mchezaji huyo amefunga mabao 110 katika mechi 352 alizocheza klabuni hapo. Msimu huu amecheza mechi 21 za Bundersligaakifunga mabao manne na kutoa pasi 11 za magoli.


BENJAMIN MENDY AGOMBEWA EPL
Klabu za Manchester United, Manchester City na Chelsea zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya beki wa kushoto wa Monaco. Mchezaji huyo amekua na wastani mzuri wa kazi za beki wa kushoto katika ligi ya mabingwa ulaya akiwazidi Marcelo na David Alaba.
Liverpool pia inaweza kujitosa katika mbio za kumuwania mchezaji huyo kutokana na ukweli kwamba ukimuondoa James Milner, upande wa beki wa kushoto hauna nguvu sana.


JESSE LINGARD ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE
Jesse Lingard amesaini mkataba wa miaka minne Manchester United wenye mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki. Lingard mwenye miaka 24 alibakiwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa awali. Mourinho mwenyewe amekiri yakuwa ni kweli Lingard anastahili mkataba mpya.


LEWANDOWSKI KUZIBA NAFASI YA ZLATAN
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameanza kumuwinda mshambuliaji staa wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, 28, kwa ajili ya kuziba nafasi ya mshambuliaji, Zlatan Ibrahimovic, 35, kama akiamua kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu.
Zlatan ameanza kuwapa wasiwasi mabosi wa United kufuatia kauli zake ambazo amekuwa akitoa katika siku za karibuni  na mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu huku klabu ya LA Galaxy ya Marekani ikiwa imeweka pesa nyingi sokoni.
Kwa sasa Mourinho anamuona Lewandowski kama mchezaji anayeendana na staili ya Zlatan na yupo tayari kutoa dau kubwa kwa ajili ya kumchukua wakati huu pia akitazamiwa kumruhusu Wayne Rooney kuondoka kikosi hapo.


CHICHARITO
Mwezi uliopita akihojiwa na BBC, Mourinho alisema, "Man United imeuza wachezaji ambao kamwe nisingewauza na kununua wachezaji ambao nisingewanunua". Haya manemo yalikua yakiwalenga Chicharito, Welbeck na Angel Di Maria. Hivi karibuni baada ya kutoka sare na Bournemouth, Mourinho amesikika akisema wakati kama huu Chicharito angekuwa na goli 20 au zaidi, tunao wachezaji wazuri lakini hawana sifa za kuleta matokeo kwa kufunga. Kauli hizi zinakazia tetesi za usajili wake.


MARCO VERRATI
Wakala wa kiungo Maco Verrati wa PSG amesema mchezaji huyo anatakiwa kuondoka kama anahitaji kushinda mataji. Kwa sasa bado ana mkataba hadi 2021, hivyo kitahitajika kiwango kikubwa cha fedha kuuvunja na Chelsea ni timu iliyoonyesha nia. Pia ikumbukwe Barcelona wanaweza kurudi tena katika mbio hizo kufuatia kuonyesha nia msimu wa mwaka jana.


ARSENE WENGER
Habari zinazovuma kwa sasa ni usemekano wa Arsenal kuwa imeshampatia Arsene Wenger mkataba wa kuinoa timu hiyo kwa misimu miwili zaidi. Kundi la mashabiki wameonyesha kutokutaka Wenger apewe mkataba mpya wa kukinoa kikosi cha Arsenal huku wengine wakibeba mabango kwenye ndege. Habari juu ya msakabali wa kocha huyo zinatarajiwa kutolewa rasmi hivi karibuni.


MICHY BATSHUAYI
West Ham imeonyesha nia ya kutaka huduma ya mshambuliaji huyu wa Chelsea kwa msimu ujao. Batshuayi bado ana miaka minne kwenye mkataba wake na Chelsea haitakua tayari kumuachia moja kwa moja kwa sababu inaamini bado ni mdogo anahitaji mechi nyingi apate uzoefu. Hivyo uwezekano uliopo ni wa mkopo wa muda mrefu (Msimu mzima).


WAYNE ROONEY
Wakala wa mchezaji Wayne Rooney wa Manchester United amesafiri kwenda nchini China kwaajili ya kufanya makubaliano na vilabu vinavyomhitaji mchezaji huyo. Kwa sasa Rooney amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza na pia umri wake wa miaka 30 umekua ni kigezo kikubwa cha ushawishi wa kuhama. Guangzhou Evergrande inayofundishwa na meneja wa zamani wa Chelsea Luiz Felipe Scolari ni moja ya timu inayohitaji huduma ya mchezaji huyo.


MESUT OZIL
"Anaweza kushinda mataji pale."
"Ikiwa anataka kushinda taji kubwa, ana nafasi nzuri kushinda akiwa Bayern."
Hizi ni kauli aliyoitoa gwiji wa soka Michael Ballack akimtaka mjerumani mwenzake Ozil kufikiria kuondoka Arsenal na kwenda Bayern Munich.
Mkataba wa sasa wa Ozil mwenye umri wa miaka 28 unaisha mwaka 2018, na bado hajasaini mkataba mpya, ambapo ikiwa ataamua kutokuongeza mkataba ni vema kwa Arsenal kumuuza msimu ujao ili wapate fedha na si kumuacha aende huru mwishoni mwa mkataba.


DE GEA AU COURTOIS KWENDA MADRID ?
Magolikipa hawa wote wana nafasi ya kuichezea Real Madrid msimu ujao kutokana na ukweli kwamba uwezo wao umekua kivutio kikubwa kwa klabu hiyo.
 
Zinedine Zidane pia angependa kuongeza nguvu msimu ujao ili kumsaidia golikipa wa Costa Rica aliyepata mafanikio makubwa katika kombe la dunia, Keylor Navas.

Ikumbukwe kuwa magolikipa hawa wote waliwahi kuichezea Atletico Madrid kabla ya kuhamia klabu za Manchester United na Chelsea.
Pia msimu uliopita paliwahi kuwa na tetesi nzito za kuhamia Madrid zilizoleta sintofahamu kubwa katika vilabu vyao.


ANTOINE GRIEZMANN
Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo ameiambia Manchester United yakuwa ni klabu ndogo na wasifikirie juu ya Griezmann kwakua haendi kokote msimu ujao.
United imemuweka Griezmann namba 1 katika orodha ya wachezaji inaotaka kuwasajili msimu ujao. Na pia imeonyesha nia ya kumpatia Griezmann jezi namba 7 iliyokua ikivaliwa na moja ya mchezaji anayependezwanae, David Beckham.


RONALD KOEMAN KWENDA BARCELONA
Kocha wa sasa wa Everton anatazamiwa kuwa kocha mpya wa Barcelona msimu ujao kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Luis Enrique.
Barcelona imekua katika kipindi ambacho imeamua kuwapatia nafasi ya ukocha wachezaji wake wa zamani ambao wanaielewa zaidi timu hiyo.
Koeman alikuwako kwenye kikosi cha dhahabu cha mkongwe Johan Cruyff, alikuwa mchezaji kwa miaka 6 na anakumbukwa kwa goli lake la ushindi katika mchezo wa kikombe cha kwanza cha ulaya kinachowakutanisha mabingwa wa UEFA na EUROPA.
Pia amejipatia sifa kubwa katika timu ya Southampton akitengeneza timu nzuri ya ushindani.

VAN DIJK
Manchester United, Chelsea, Liverpool, Manchester City na PSG ni timu zinazomuwania beki huyu mwenye umri wa miaka 25 kutoka Southampton katika dirisha dogo la usajili.
Kutokana na uwezo wake klabu yake imempatia nafasi ya ukepteni kufuatia kuondoka kwa Fonte aliyetua mwezi Januari kuiongoza timu, kwa kuikubali nafasi hiyo timu imejihakikishia kuwanae hadi mwisho wa msimu huu.
Kwa uwezo alionao ingawa ana mkataba wa miaka mitano, kwa nguvu ya fedha vilabu hivi hakika vitarudi tena msimu ujao kuitaka sahihi yake.

0 comments:

Post a Comment