UTI (URINARY TRACT INFECTION)
U.T.I ni nini ?
U.T.I ni maambukizi katika njia za mfumo wa utoaji taka mwili kwa kupitia mkojo.
Unaathiri zaidi wanawake, ila wanaume na watoto pia wanaupata.
-Tatizo hili hutokea pale mlango wa njia ya haja ndogo unaposhambuliwa na vimelea ambao husambaa na wasipotibiwa mapema huenea hadi kwenye figo na athari zake ni mbaya.
Njia ya mkojo ni ipi ?

Kwa ujumla njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa mwanaume na mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS. Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu.
Kibofu kikipata maambukizi ugonjwa unajulikana kama CYCITITIS. Baada ya kibofu inafuata mirija miwili inayokwenda kwenye figo mbili. Mirija hii inaitwa URRETERS na ikishaambukizwa inajulikana kama URRETITIS. Na mwisho wa njia ya mkojo ni figo mbili yaani KIDNEYS na hizi figo zikishaambukizwa ugonjwa unajulikana kama NEPHRITIS.
Vimelea wa aina gani wanaoleta ugonjwa wa UTI.

Vimelea katika makundi maalum vinavyojulikana ni kama ifutavyo:
1. BACTERIA eg Streptococci, Staphylococci, E.Coli, H.Influenza, Proteus sp.Pseudomonas etc.
2. VIRUSES eg Clamydia tracomatis
3. FUNGI eg Candida albicans
4. TRICHOMONIASIS
5. SCHISTOSOMIASIS (kichocho)
6. PARASITES
7. GONORRHEA (kisonono).
Njia za Maambukizi:
1) Kuoga maji machafu hasa ya mabwawani (ambapo wanyama huingia) au kisimani yaliyotokana na kuchotea ndoo ya kufulia yenye vimelea hivyo.
2) Kuchangia nguo za ndani (boksa, taiti au chupi), na za kuogea (mataulo au kanga).
3) Kujamiiana bila usalama (kwa kufanya ngono zembe) wanapata magonjwa ya zinaaa kwa urahisi na hivyo wanakuwa tayari wana UTI.
4) Kutokuzingatia usafi wa nguo za ndani (hata mara tunaponunua nguo za mitumba).
5) Mazingira hatarishi ya vyoo vyetu kwa kujaa ama kutokuvisafisha mara kwa mara.
6) Kutawaza kwa kuvutia maji kuelekea kwenye njia ya mkojo (nyuma kwenda mbele).
7) Watoto wadogo mara nyingi wanapata UTI kutokana na kutobadilisha nepi kwa wakati na hivyo unyevu wa mikojo na mavi huvuta vimelea na kuleta maambukizi.
Dalili:
Dalili za UTI zinaonekana kulingana na aina ya maambukizi. Lakini dalili kuu kwa watoto na watu wazima zinafanana nazo ni;
1) Maumivu wakati wa kukojoa na kwenye viungo vya mfumo wa mkojo (chini ya kitovu).
2) Kuhisi haja ya kukojoa kila wakati (katika hatua za mwanzo unaweza kukojoa kidogo).
3) Kusisimka wakati wa kukojoa hata kuhisi baridi.
4) Kutoa mkojo mchafu au usaha kwenye njia ya mkojo.
5) Kulia, homa hadi kutapika hasa kwa watoto ni dalili rahisi za kugundua maambukizi kwa watoto wadogo.
Athari:
Athari za UTI nazo ziko nyingi na zinategemeana na aina ya maambukizi. Ugonjwa huu ukikaa kwa muda mrefu huwea kuathiri figo.
Figo isipofanya kazi hutokea;
- Mlundikano wa taka mwili.
- Mashambulizi ya magonjwa mengine kwa urahisi.
- Kutokwa na haja ndogo kwa wingi hivyo kupoteza maji mengi.
- Kuhisi kiu mara kwa mara.
- Gharama za matibabu kuongezeka.
- Kupoteza nguvu kazi (kwa kuugua kwa muda mrefu, kupata utaahira au kufa).
Tiba:
Matibabu nayo yako mengi na tofauti kulingana na aina ya maambukizi.
1) Fika hospitali mapema kwani tiba yake ipo (Anti-biotics).
2) Kunywa maji mengi pamoja na juisi itokanayo na matunda halisi.
3) Kunywa maji meng au kwenda haja ndogo mara baada ya kujamiiana.
4) Tiba asili ni kama vile; kijiko cha baking soda, zabibu nyeusi na nyekundu, nanasi, kitunguu swaumu, limau/ ndimu, unga wa majani ya mlonge, mshubiri (Aloe-vera) n.k
Muhimu:
U.T.I hutoweka baada ya siku 3 hivi baada ya kutumia tiba asili kwa siku 2 au 3, vinginevyo utakua umekomaa, nenda hospitali mara moja.
Ushauri:
1) Kunywa maji ya kutosha kila siku (husadia kuwatoa vimelea kwa kwenda haja ndogo mara kwa mara).
2) Matikiti ni matunda yanayoshauriwa kuliwa kwakua yatakupatia maji pia.
3) Hakikisha unajisafisha vizuri mara baada ya kwenda haja.
4) Hakikisha unabadilisha mara kwa mara nguo yako ya ndani, hasa kwa akina mama.
5) Usikae na haja ndogo muda mrefu, nenda ukajisaidie kadri unavyojisikia.
6) Epuka kuchangia ama kurithishana nguo za ndani, mataulo au kanga na hakikisha unazifua.
7) Punguza unywaji wa pombe na vinywaji vingine vyenye sukari, kwasababu sukari ni chakula cha bakteria hivyo kwa kuendelea kunywa vinywaji vyenye sukari kutafanya hali kuendelea kuwa mbaya.
Dayati (Mlo kamili) Muhimu Kudhibiti U.T.I:
- Pendelea kula vyakula na kunywa vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Vitamini C ambavyo utavipata kwenye matunda ya aina mbalimbali yakiwemo; machungwa, mboga za majani, epo, tikitimaji na nanasi.
- Jiupushe na vyakula vya 'kupaki' kama vile 'chizi', chokoleti na bidhaa zingine zinazotengenezwa kutokana na maziwa.
- Pia jiepushe na ulaji wa vyakula vyenye viungo vingi kama pilau; epuka vinywaji vyenye 'Caffeine', kilevi na sigara na mwisho achana na vinywaji kama soda na vinavyofanana na soda.

HOMA YA INI
Ugonjwa wa homa ya Ini maarufu kama
Hepatitis B umetajwa kuwa maambukizi yake ni makubwa na ya haraka zaidi ya
Ukimwi.
Kwa mujibu
wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) yanaonyesha kuwa kiwango cha
maambukizi ya Homa wa Ini B kwa Taanzia ni wastani wa watu 8 katika kila watu
100.
Wakati
maambukizi ya Ukimwi ikiwa ni watu 5 katika kila watu 100.
Katibu Mkuu
wa Serikali, Dr. Mpoki Ulisubisya amesema Serikali imeanza kuwatumia watafiti
wake ili kuangalia kwa undani kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

0 comments:
Post a Comment