SAFU YA ULINZI TAIFA STARS INATIA MATUMAINI
Rekodi zinaonyesha kwamba Taifa Stars ina ukuta usiopitika kirahisi. Timu hiyo iliifunga Botswana kwa mabao 2-0 jana Jumamosi na kuwa na rekodi ya kuruhusu bao moja tu katika mechi nne zilizopita.
Katika mechi hizo, Stars ilipata suluhu na Lesotho katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya Cosafa kabla ya baadaye kupata ushindi wa penalti.
Baada ya hapo Stars ilicheza na Rwanda katika mechi ya kufuzu CHAN na kupata sare ya bao 1-1 jijini Mwanza kabla ya kupata suluhu katika mechi ya marudiano mjini Kigali.
Stars ilithibitisha kuwa ukuta wake uko vizuri baada ya jana kutoruhusu bao dhidi ya Botswana.
"Nilianza kwa kuijenga timu kuanzia kwenye ulinzi kwenda mbele, nadhani sasa tunakwenda vizuri. Timu inafanya vizuri katika ulinzi," alisema kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga.
MSUVA, OKWI KUMEKUCHA
Nyota wa Taifa Stars, Saimon Msuva ameonyesha kwamba ni hatari katika kufunga baada ya kukimbizana na staa wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Emanuel Okwi.
Msuva aliifungia Stars mabao yote mawili wakati ikiilaza Botswana 2-0 jana Jumamosi hivyo kufikisha idadi ya mabao matatu katika mechi mbili za mwisho alizocheza.
Kabla ya kujiunga na Stars, Msuva alitoka kuifungia timu yake ya Difaa El Jadida ya Morocco bao moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya CR Khemis Zemamra.
Hata hivyo Msuva anakimbizwa na Okwi ambaye amefunga mabao matano katika mechi mbili za mwisho alizocheza. Okwi aliifungia Simba mabao manne katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kabla ya kuifungia Uganda bao pekee la ushindi dhidi ya Mirsi juzi Ijumaa.
TAARIFA ZA TIMU MBALIMBALI KWA WADAU
SIMBA SC
'Mwadui poleni':
Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui, mabao yaliyofungwa na Emmanuel Okwi (7, 67) pamoja na John Bocco (72).Okwi alifunga bao la mapema baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shiza Kichuya kisha kuupiga mpira uliompita kipa wa Mwadui, Anord Masawe.
Kikosi Simba: Aishi Manula, Ally Shomary, Mohamed Husein 'Tshabalala', Juuko Murshid, Salim Mbonde, James Kotei, Shiza Kichuya, Mdhamiru Yassin, John Bocco, Emmanuel Okwi, Nicholas Gyan.
Mwadui:
Anold Masawe, Malika Ndeule, David Luhende, Revocatus Mgunga, Abdallah Mfuko, Razack Kharfan, Abdallah Seseme, Awadh Juma, Evarist Mjwahuki, Gerald Mathias/ Benedictor Mwampyate, Hassan Kabunda.
Timu hiyo ilianza wa kishindo Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku Emmanuel Okwi akiandika rekodi ya kufunga hat trick. Kisha ikatoka sare dhidi ya Azam F.C
YANGA FC
*********** BINGWA MSIMU WA 2016/2017 **********
*********************************************
IBRAHIM AJIB ASAINI RASMI KLABU YA YANGA
Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, straika Ibrahim Ajib amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu.
Ajibu amesaini mkataba huo leo mbele ya mabosi wa Yanga na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Nyota huyo anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Yanga katika usajili wa sasa huku klabu hiyo ikiwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi.
AZAM
KAWEMBE MGUU NJE, MGUU NDANI
Mtendaji Mkuu wa Azam, Sady Kawemba amesema taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya jamii kuwa ataachana na timu hiyo siyo za kweli.Kawemba amesema kwa sasa yupo katika mazungumzo na klabu hiyo na muda utakapofikia ataweka kila kitu wazi na si kama sasa taarifa zilivyokuwa zimeenea.
Kawemba alisema mkataba wake na Azam unakaribia kumalizika ila kwa sasa wapo katika mazungumzo na wakurugenzi wa timu hiyo na kama watafikia muafaka ataendelea kubaki na kama wakishindwana ataangalia maisha mengine.
"Nipo katika majukumu yangu ya kawaida ndani ya klabu kama nilivyosema hapo awali kwani kocha amenikabizi ripoti na nimeshaanza kuifanyia kazi kama mtendaji mkuu wa timu huku nikiwa nasubili hatma yangu ndani ya klabu kuwa nini kinafaata," alisema Kawemba.
Meneja mkuu wa Azam, Abdul Mohamed alisema suala hili lipo ndani ya uongozi na jambo hili hawataliweka wazi mpaka hapo litakapokamilishwa na uongozi wa klabu hiyo lakini kwa sasa bado ni mapema kulielezea.
Mahali Ilipo: Kata ya Tungi, Mtaa wa Magogoni.
Uwanja Ulipo: Karibu na barabara kakikati ya vituo vya Chadibwa na Makaburini.
Habari:
Ligi Ya Mnadani:
Mkunazini.
Mkunazini ni bingwa wa ligi ya MNADANI CUP, imepata zawadi ya Laki moja (100,000/=) na mpira mmoja.
Mechi za Kirafiki:
Kwa sasa timu inajiandaa na mchezo wa fainali utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 16/7/2017 katika uwanja wa wa Jakaya Kikwete Stadium (Kidongo Chekundu).
Mashindano:
Mkunazini itashiriki mashindano ya Mazingira Cup katika uwanja wa Geza na mechi ya mzunguko wa kwanza kundi itakua jumanne ya tarehe 18/7/2017 dhidi ya Geza Juu.
Michezo mingine:
Ijumaa hii tarehe 7/7/2017 kutakua na mechi ya timu za wiki mazoezini ikiambatana na zawadi kwa wachezaji.
Mechi za Kirafiki:
Kwa sasa timu inajiandaa na mchezo wa fainali utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 16/7/2017 katika uwanja wa wa Jakaya Kikwete Stadium (Kidongo Chekundu).
Mashindano:
Mkunazini itashiriki mashindano ya Mazingira Cup katika uwanja wa Geza na mechi ya mzunguko wa kwanza kundi itakua jumanne ya tarehe 18/7/2017 dhidi ya Geza Juu.
Michezo mingine:
Ijumaa hii tarehe 7/7/2017 kutakua na mechi ya timu za wiki mazoezini ikiambatana na zawadi kwa wachezaji.








0 comments:
Post a Comment