Mambo yameiva kwa wakazi wa Kigamboni, hii ni sehemu ya majengo ya utakao kuwa mji mpya wa Kigamboni kwa mujibu wa Mtandao wa Wizara husika.
Eneo hili litahusu maeneo ya makazi yasasa ambayo yanakaliwa na watu. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali la Mwaka 2008 wakazi wa kata zipatazo tano watafidiwa kuhamishwa kupisha mradi huu.
Eneo litakalo chukuliwa ni la Kigamboni likichukua zaidi ya kata tano ambazo ni Kigamboni, Vijibweni, Somangila, Mji Mwema na Kibada. Eneo hili lina wakazi wapatao 82,808 ambao watafidiwa kulingana na sheria na taratibu zilizowekwa.



0 comments:
Post a Comment