KITAIFA: Brazil yaisamehe Tanzania mabilioni ya fedha ya mwaka 1979. Kamanda Mambosasa amtaka polisi anayejiita Faru john. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa akamatwa na polisi baada ya kumkaribisha mkuu wa mkoa kwenye kikao cha kijiji akiwa amelewa. Bunge lahitimishwa watanzania wakishuhudia kheri na vitimbwi. Kina Manji wasomewa mashtaka saba wakiwa muhimbili. Sakata la mimba shuleni latua kwa ma-DC. Majaliwa: Marufuku kusafirisha chakula nje ya nchi. Bakwata yalaani mauaji Kibiti. JPM kuzindua viwanda Pwani leo katika ziara ya siku 3 inayoanza mkoani humo. Kamusi Kuu ya kiswahili yapitishwa Bungeni. ********** KIGAMBONI: Hali ya hewa ni ya baridi kiasi na upepo, wananchi washauriwa kuwa makini na upepo, vumbi wakati wa mchana na baridi wakati wa usiku. **********KIMATAIFA: Boti yazama, 6 wafa, 20 wakimbizwa hospitali Colombia. **********BIASHARA: Sekta ya Benki yaanza kuona nuru mpya. Rangi itakuongezea au kukupunguzia wateja katika biashara yako. Mazingira ya biashara yaboreshwe kukuza uchumi, kuondoa umasikini. Shilingi 50 yaanza kupoteza bidhaa za kuendananazo baada ya wafanyabiashara wengi kutengeneza zaidi vitu vya shilingi 100. *********MICHEZO: *** UEFA: Timu za EPL zaanza vyema mzunguko wa kwanza. Diego Costa aachwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa chelsea watakaoshiriki UEFA hatua ya makundi. Zlatan Ibrahimovic ajumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa Man United watakaoshiriki UEFA hatua ya makundi. Real Madrid bingwa. ENGLAND: Chelsea bingwa EPL, Conte achaguliwa kocha bora wa msimu. . ******** LA LIGA: Real Madrid bingwa la liga. ******* USAJILI: Lacazette kumfikirisha upya Sanchez juu ya kuihama Arsenal. Atletico yamtaka Diego Costa kutulia Chelsea hadi Januari.*********** AFRIKA: Ligi ya vilabu bingwa Afrika iko katika hatua ya makundi. AFCON 2017; Cameroon alitawazwa kuwa Bingwa baada ya kuifunga Misri goli 2-1 katika fainali na sasa inacheza kombe la mabara. ******** Pata habari hizi na nyinginezo nyingi kupitia habari zetu za michezo za kimataifa. ********. TANZANIA: *** Simba yazidi kufanya kweli. Msuva aipaisha TZ. TRA: Klabu za soka zilipe kodi. *** KIGAMBONI: Uhaba wa ligi ndani ya Wilaya ya Kigamboni umezorotesha uibuaji wa vipaji na kudumaza viwango vya wachezaji waliopo. Wadhamini waombwa kujitokeza kuanzisha ligi mbalimbali wilayani humo ili kuwaokoa vijana wengi na mambo mabaya. Katika uwanja wa Mnadani karibu na maeneo ya Tungi kwa kasilati ligi ambayo inakusanya wachezaji wengi kwa sasa imeisha kwa Mkunazini kuibuka bingwa katika fainali baada ya miaka mingi kupita. Ligi ya Eid El Fitr yaendelea katika hatua ya robo fainali leo 20/6/2017, katika uwanja wa machava.

KIGAMBONI NA MAMBO YA ELIMU

TUZUNGUMZIE SHULE YETU YA SEKONDARI KIDETE
Hadi kushika mkia !!
Tuamke Usingizini, Haya yalitokea.
Dar es Salaam, Wilaya ya Kigamboni.
Shule ya sekondari Kidete ya Dar es Salaam, ndiyo iliyoshika mkia kitaifa katika matokeo ya mtihani kidato cha nne 2016.
Shule hiyo iliyopo umbali wa kilometa 10 kutoka daraja la Mwalimu Julius Nyerere katika Wilaya ya Kigamboni, matokeo yake yamewashangaza baadhi ya wanafunzi na walimu.
Mwandishi kutoka Mwananchi alifika katika shule hiyo saa 9:34 alasiri, muda wa masomo ukiwa umekwisha na wanafunzi wengi walikuwa wameondoka, lakini walikuwapo wachache waliokuwa wakijisomea. Miongoni mwa wanafunzi hao, Salma Said ambaye anasoma kidato cha nne mchepuo wa Sayansi, alisema taarifa za shule yao kuwa ya mwisho kitaifa zimewafikia, lakini bado hajaziamini.
“Hapa kuna walimu takribani 25 na wanajitahidi sana kufundisha mpaka muda wa ziada, huenda matokeo hayo yametokana na wanafunzi wenyewe, lakini si walimu. Hata mazingira ya shule ni rafiki kwa kujifunza,” alisema Salma.
Mwanafunzi mwingine, Iddy Omary wa kidato cha nne mchepuo wa Sanaa alisema Kidete haikuwahi kuwa miongoni mwa shule za mwisho, hata kama ilikuwa haifanyi vizuri si kwa kiwango hicho kilichowashtua.
“Miundombinu ya shule ni mizuri na waalimu wanajitahidi kufundisha hata wanafunzi walikuwa wanaonyesha jitihada katika masomo, licha ya kwamba baadhi yao hawakuwa na nidhamu sana,” alisema Omary.
Mwalimu mmoja ambaye alikutwa shuleni muda huo, kwa sharti la kutotajwa jina gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema amejisikia vibaya kuona shule hiyo inakuwa ya mwisho kitaifa. Alisema hadi muda huo alikuwa amepokea pole nyingi kutoka kwa marafiki na walimu wenzake.
“Sikuwahi ‘kufelisha’ wanafunzi, nimehamia hapa miaka ya karibuni, hata huko nilikotoka sikuwahi kupata rekodi mbovu kama hii,” alisema mwalimu huyo. Alisema changamoto kubwa katika shule hiyo ni ufaulu mdogo wa wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza na umbali wa shule kwa wanafunzi walio wengi ambao husababisha kufika kwa kuchelewa na kuwa na muda mfupi wa masomo.
“Wanafunzi wengi hapa wanatoka Yombo Buza na maeneo mengine ya Wilaya ya Temeke wakati mwingine wanafika hapa saa tatu asubuhi wakiwa wametoka nyumbani saa 10 au 11 alfajiri na inabidi waondoke saa 8:30 mchana ili wawahi kufika nyumbani,” alisema mwalimu huyo. Alisema suala la umbali wa wanafunzi hupunguza uwezo wao wa kujisomea kwani huchoka hivyo kuishauri Serikali izingatie umbali wa wanafunzi wakati wa kuwapangia shule.

0 comments:

Post a Comment